Unknown Unknown Author
Title: SHIRIKA LA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII PSPF LINDI YATOA MSAADA WA THAMANI YA TSH MILIONI 45,000/= JIMBO LA MCHINGA, LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi  akipokea msaada wa madawati 90 yaliyotolewa na Pspf,Anaekabisdhi  msaada huo ni Men...
PSPF Lindi
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi akipokea msaada wa madawati 90 yaliyotolewa na Pspf,Anaekabisdhi msaada huo ni Meneja wa PSPF Lindi Bw Mtumwa Ramadhan.,Msaada huo ulikabidhiwa katika kijiji cha Chilala,Lindi Vijijini
PSPF Lindi
Picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa misaada mbalimbali,Kutoka kushoto, Mzee Ng'ombo, (Diwani wa kata ya Rutamba), Patrick Mtomase, (Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya wananchi Chilala), Mtumwa Ramadhan, (Meneja Pspf Lindi), Abdu Makwita, (Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lindi) na Bw Bakari Omary, (Katibu TSD wilaya ya Lindi)
Chilala Lindi Vijijini
Wanafunzi wa chuo cha maendeleo ya wananchi Chilala Lindi Vijijini
PSPF Lindi
Meneja wa PSPF Akikabidhi msaada wa Komputa na Printa kwa ajili ya Ofisi ya TSD wilaya ya Lindi anaepokea ni katibu wa TSD bw Bakary Omary

Na Abdulaziz LindiJumla ya madawati 90 yenye thamani ya Ths milioni 45,000/=  yametolewa na shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii PSPF kwa mbunge wa jimbo la mchinga Saidi Mtanda kwa ajili ya shule za msingi katika jimbo.

Akikabidhi madawati hayo meneja wa PSPF Lindi Mtumwa Ramadhani kwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Lindi Abdu Makwita kwa niaba ya mbunge wa mchinga Saidi Mtanda alisema alieleza kuwa mfuko wa PSPF unatambua changamoto zinazoikali sekta ya elimu wilayani humo na kupitia mpango wa kusaidia Jamii kwa kushirikiana na wadau wengine wanao changia elimu tumeona ni vyema kusaidia ili kupunguza matatizo hayo.

Mtumwa alisema kuwa msaada huo wa madawati hayo utatumika ipasavyo na kuongeza hali ya usikivu kwa wanafunzi na kuinua kiwango cha taaluma shuleni hapo ikiwa pamoja na wanafunzi kupenda kukaaa darasani.

Aidha alibainisha kuwa mfuko wa PSPF umeanzisha mpango wa uchangiaji wa hiari kwa lengo la kupanua wigo kwa wanachama walioajiriwa na waliojiajiri katika sekta rasmi na isiyo rasmi ili kuwawezesha watu ambao hawakuweza kupata huduma za mfuko pasipo ajira rasmi.

Mpango wa uchangiaji wa hiari Mwanachama hatakuwa huru kuchagua jinsi ya kuchangia kwa kuwasilisha michango yake, wiki, mwezi, Au msimu kutegemea na hupatikanaji wa kipato chake cha ziada kwa ajili ya akiba. Hivyo mnaotusikia mnaweza kufika katika ofisi zetu kwa Uandikishwaji, Alibainisha Mtumwa.

Pspf inatoa mafao katika mpango huo wa hiari jumla ya mafao sita ambayo ni mafao ya elimu, ujasirimali, uzeeni, kifo, ugonjwa na ulemavu na fao la kujitoa ambalo mwanachama atalipwa asilima 100 ya akiba yake pamoja na riba pindi atakapo jitoa uanachama.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri Abdu Makwita alisema msaada wa madawati hayo umekuja kwa wakati kwani shule zilizo katika wilaya hiyo zina upungufu wa madawati zaidi ya 1000 na kusababisha wanafunzi wengi kukaa chini.

Makwita alisema mbunge wa jimbo la mchinga Saidi Mtanda ameaandaa mkakati wa kuondoa tatizo la madawati kwa awamu ya kwanza kutengeneza madawati zaidi ya 300 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ambayo yatolewa kwa shule zenye upungufu mkubwa wa madawati kwa sasa.

Aidha pamoja na jitihada za mbunge wa jimbo hilo na wadau wa elimu pia halmashauri imejipanga na kuandaa mkakati wa kuboresha elimu kwa kuhakikisha kuondoa changamoto zinazohikabili sekta hiyo ikiwemo upungufu wa madawati, vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na vyoo.
"kutokana na mikakati hiyo halmashauri inatarajia kuendesha mikutano na vikao vya uamashishaji wadau elimu kwa kuwa kumbusha umuhimu wa kuchangia elimu kwa manufaa ya watoto wao ili elimu iboreke kufuatana na kukua kwa Uchumi wa Mikoa ya kusini.

Sambamba na madawati hayo, Pspf pia imetoa komputa moja na Printa kwa ajili ya Ofisi ya chuo cha maendeleo ya wananchi Chilala pamoja Kompyuta moja na Printa kwa Ofisi ya Tsd wilaya ya Lindi

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top