Unknown Unknown Author
Title: HIKI NI KITU KINGINE KIPYA KUTOKA KWA DIAMOND PLATNUMZ KUENDELEA KUPIGA HELA KUPITIA MZIKI WAKE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Diamond Platnumz ni msanii mwengine mkubwa wa Kitanzania aliyejiunga na Mkito.com kwa ajili ya kusambaza muziki wake mtandaoni. Msanii h...
Diamond Platnumz ni msanii mwengine mkubwa wa Kitanzania aliyejiunga na Mkito.com kwa ajili ya kusambaza muziki wake mtandaoni. Msanii huyu anajiunga na wengine kama Fid Q, Nay Wamitego, Rich Mavoko, Vanessa Mdee, Juma Nature, Barnaba, Linah, Belle 9 na wengine wengi katika mchakato unaoendelea kuwawezesha wasanii kujipatia kipato kutokana na muziki wao kupakuliwa kwenye mtandao. 
Diamond kabla ya kuondoka kuelekea Afrika ya Kusini kwaajili ya video yake mpya aliona ni vyema kuungana na Mkito.com kwani ni kampuni ya Kitanzania yenye madhumuni mazuri kwa tasnia ya muziki nchini. Watumiaji wote wa Mkito.com sasa wanaweza kupata nyimbo za Diamond kupitia www.mkito.com ikiwemo albam ya Best Of Diamond na pia wimbo wake mpya Mdogomdogo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top