Unknown Unknown Author
Title: TIMU YA FC VITO YA RUANGWA - LINDI, YAAGWA RASMI LEO KWENDA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO CHINI YA MIAKA 10 NCHINI FINLAND
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Naibu waziri wa Tamisemi,  mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa akikabidhi bendera ya taifa kwa timu ya Vito Fc ya Ruangwa Na Abdulaziz ...
TIMU YA FC VITO YA RUANGWA
Naibu waziri wa Tamisemi, mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa akikabidhi bendera ya taifa kwa timu ya Vito Fc ya Ruangwa

Na Abdulaziz ,Video
Wizara ya habari utamaduni na michezo imekabidhi bendera ya Taifa kwa timu ya mpira wa miguu ya wasichana chini ya ya miaka 10 ya Fc Vito malaika ya wilayani ruangwa mkoani Lindi itakayoshiriki kombe la dunia la watoto mashindano yatakayochezwa nchini Filand hivi karibuni.

TIMU YA FC VITO YA RUANGWA
Akiaga timu hiyo kwa niaba ya wizara hiyo, Naibu waziri wa Tamisemi elimu ambae pia ni mbunge wa Ruangwa, Kassim majaliwa alieleza kuwa timu iliyoundwa toka kwa wanafunzi wa shule za msingi za wilayani humo na kufadhiliwa na mfuko wa michezo Kwa wote itaondoka ikiwa na wachezaji 12 mwalimu na mlezi wao.
TIMU YA FC VITO YA RUANGWA
Aidha majaliwa alitoa shukrani kwa wazazi wa watoto hao kwa kuridhia safari ya watoto hao huku akiwataka watoto hao kupeperesha vema bendera ya Tanzania kwa kurudi na ushindi.
TIMU YA FC VITO YA RUANGWA
Awali  akimkaribisha naibu waziri mratibu wa safari hiyo mkurugenzi wa kituo cha michezo Kwa wote Mohamed Chigogolo mafanikio watakayopata watoto hao baada ya kushiriki mashindano hayo ni pamoja na watoto hao kupata msaada wa kusaidiwa kimasomo na wazazi wa Finland walioamua kutoa msaada huo.TIMU YA FC VITO YA RUANGWA
Sambamba na mashindano hayo watoto hao wakiwa nchini humo watajifunza lugha, kuogelea pamoja na kuangalia vivutio mbalimbali

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top