Unknown Unknown Author
Title: MELI YA JAPAN YALIPUKA BAHARINI NA KUJERUHI WATU KADHAA... SOMA HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mlipuko mkubwa umetokea kwenye meli kubwa ya mafuta nchini Japan katika Pwani ya Kusini Magharibi mwa bandari ya Himeji na kusababisha mtu...
Meli ya japan Iliyolipuka
Mlipuko mkubwa umetokea kwenye meli kubwa ya mafuta nchini Japan katika Pwani ya Kusini Magharibi mwa bandari ya Himeji na kusababisha mtu mmoja kati ya wanane waliokuwa ndani ya meli hiyo kupotea huku wengine wanne wakijeruhiwa vibaya.
Meli ya japan Iliyolipuka
Moto mkubwa ulilipuka katikati ya bahari ambapo meli hiyo yenye uzito wa tani 998 iliyokuwa ikitokea mji wa Hiroshima kuachwa ikielea ndani ya maji baada ya ajali hiyo na baadae kufatwa na meli za kupambana na majanga ya moto.
Meli ya japan Iliyolipuka
Watu saba wameokolewa katika ajali hiyo mbaya, wanne wakiuguza majeraha ya moto kwa mujibu wa shirika la habari la NHK, ambapo kapteni wa meli hiyo amesema uchunguzi kumtafuta mtu mmoja aliyepotea bado unaendelea.

Afisa usalama katika Pwani hiyo Koji Takarada amesema chanzo cha mlipuko huo bado hakijajulikana ambapo shirika la habari NHK limeripoti kuwa wafanyakazi wa meli hiyo walikuwa wakifanya kazi chini ya meli wakati mlipuko unatoke.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top