Unknown Unknown Author
Title: UEFA CHAMPIONZ LIGI: CHELSEA YAPIGWA 3-1 NA PSG!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Paris Saint-Germain, wakicheza Uwanja wa Nyumani “Parc des Princes” huko Paris, France, Usiku huu wameichapa Chelsea Bao 3-1 katika Mechi y...

clip_image001Paris Saint-Germain, wakicheza Uwanja wa Nyumani “Parc des Princes” huko Paris, France, Usiku huu wameichapa Chelsea Bao 3-1 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

clip_image001[5]Ezequiel Lavezzi alitangulia kuwapa PSG Bao la kuongoza katika Dakika ya 4 baada kuweka gambani Mpira uliookolewa kwa Kichwa na John Terry na kufumua Shuti moja kwa moja na kumpita Kipa Petr Cech.

clip_image001[7]Chelsea walisawazisha kwa Penati ya Dakika ya 27 iliyopigwa na Eden Hazard na ilitolewa na Refa Milorad Mazic kutoka Serbia alipoamua Sentahafu wa PSG Thiago Silva ‘kamwangusha’ Oscar.

Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 1-1.

clip_image001[9]PSG walifunga Bao lao la 2 baada ya Ezequiel Lavezzi kupiga Frikiki safi ambayo Kipa Petr Cech alishindwa kuzuia na kumparaza Zlatan Ibrahimovic kisha Mchezaji wa Chelsea David Luiz kuusindikiza wavuni.

clip_image001[11]Nchezaji alietoka Benchi, Javier Pastore, aliipa PSG Bao la 3 katika Dakika ya 90 baada ya kupokea Mpira wa kurushwa na kuwatoka Cesar Azpilicueta, Frank Lampard na John Terry kisha kupiga Shuti la chini chini na kumshinda Kipa Petr Cech.

Timu hizi zitarudiana huko Stamford Bridge Jumanne Aprili 8.

VIKOSI:PSG: Sirigu, Jallet, Alex, Thiago Silva, Maxwell, Verratti, Thiago Motta, Matuidi, Cavani, Ibrahimovic, Lavezzi.

Akiba: Douchez, Cabaye, Marquinhos, Digne, Rabiot, Pastore, Lucas Moura.

CHELSEA: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Luiz, Willian, Oscar, Hazard, Schurrle.

Akiba: Schwarzer, Lampard, Torres, Mikel, Ba, Ake, Kalas.

REFA: MILORAD MAZIC (SERBIA)

 

UEFA CHAMPIONZ LIGI ROBO FAINALI

Marudiano [Saa 3 Dak 45 Usiku]

Jumanne Aprili 8

Chelsea v Paris Saint-Germain [1-3]

Borussia Dortmund v Real Madrid [0-3]

Jumatano Aprili 9

Bayern Munich v Manchester United [1-1]

Atletico Madrid v Barcelona [1-1]

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top