Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA MKOA WA LINDI APOKEA MSAADA WA MADAWATI 110 KUTOKA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI (TPA)
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Mkoa Ludovick Mwananzila akipokea Msaada wa madawati 110 kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Ndg: Absalom...

MADAWATI MAHUMBIKAMkuu wa Mkoa Ludovick Mwananzila akipokea Msaada wa madawati 110 kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Ndg: Absalom Bohella, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi ndg Nassor hamid akishuhudia makabidhiano hayo. MADAWATI MAHUMBIKA.4Mkuu wa Mkoa akiwa katika Picha ya Pamoja na Wadau mbalimbali walihudhuria hafla hiyo ya Makabidhiano ya Msaada wa Madawati kutika Kwa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari TPA.MADAWATI MAHUMBIKA.5Kutoka Kulia: Mkuu wa wilaya ya lindi ndg:Nassor Hamidi, Mkuu wa Mkoa walindi Ndg:Ludovick Mwananzila, Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya usimamizi wa Bandari Ndg: Absalom Bohella, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Lindi Ndg: Ngaweje na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Ndg: Matei Makwinya

NA. ABDULAZIZI VIDEO, LINDI

SHULE mbalimbali zikiwemo za msingi na Sekondari,mkoani Lindi,
zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati, yapatayo 32,476, jambo
ambalo linawasababishia idadi kubwa ya wananfunzi kulazimika kusoma
wakiwa wameketi sakafuni.

Mkuu wa mkoa huo, Ludovick Mwananzila ameyaeleza hayo jana alipokuwa akipokea kutoka mamlaka ya usimamizi wa Bandari (TPA) msaada wa madawati 110 yenye thamani ya TSh. 20.0 milioni, hafla ambayo imefanyika viwanja vya Shule ya msingi, Mahumbika, Lindi vijijini.

Katika msaada huo, uliotolewa na (TPA) Halmashauri ya Lindi vijijini,
imepatiwa idadi ya madawati (67) wakati Manispaa, imesaidiwa madawati (47).
MADAWATI MAHUMBIKA.3Akizungumza na wananchi katika hafla ya kupokea msaada huo, Mwananzila amesema mahitaji ya madawati kwa mkoa wake ni, 68,907 wakati yaliyopo ni 36,431 tu, na kufanya upungufu wa madawati 32,476.

Mwananzila amesema kwa upande wa Shule za msingi kuna upungufu wa
madawati (21,988) wakati zile za Sekondari nazo zinakabiliwa na
upungufu wa madawati (10,488).

Alifafanua kwa kusema Halmashauri ya Lindi vijijini inaoongoza kwa
upungufu wa madawati (6,427), ikifuatiwa na Nachingwea yenye madawati (8,584) na kufanya upungufu (6,904) sawa na asilimia 40.58, Ruangwa mahitaji ni,11,802 lakini yaliyopo ni 9,211 na kufanya pungufu 2,591 sawa na asilimia 31.91.

Kilwa mahitaji ya madawati ni,10,605,yaliyopo ni (9,026) na kufanya
pungufu (1,579) sawa na asilimia 14.89, Liwale inaupungufu wa madawati
(1,984) wakati mahitaji ni 7,799 huku yaliyopo 5,815,
Manispaa ya Lindi, inayo madawati 3,677 wakati mahitaji ni 6,180 na kufanya pungufu 2,503.

Mwananzila akasema baada ya kuliona tatizo hilo, aliamua kuandika
barua kwa wadau mbalimbali wa maendeleo,wakiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) wausaidie mkoa huo,kuupatia msaada wa madawati ili kupunguza tatizo la wanafunzi kuketi sakafuni wakati wa masomo yao.

"Baada ya kuliona hilo, niliamua kuandika barua kwa wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na mamlaka ya TPA, watusaidie na kufanikiwa madawati haya 110"Alisema Mwananzila.

Pia ameagiza yatunzwe madawati hayo, ili yaweze kuchukuwa muda mrefu wa kuishi, ikiwemo yawasaidie na wanafunzi wengine watakaoanza masomo kwenye Shule za mkoa huo.MADAWATI MAHUMBIKA.2Awali akitoa taarifa fupi, kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya
usimamizi wa Bandari mkoani Mtwara, Absalom Bohella, alisema TPA ikiwa ni taasisi nyingine ya Serikali, kwa sasa ipo katika mpango kabambe wa matokeo makubwa (Big Result Now) unaotaka kuongeza kasi na ufanisi wa majukumu yake, na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.

Bohella alisema TPA, inayotoa huduma zake kwa ufanisi na viwango vya
juu ili kuinua pato la Taifa, liweze kuhudumia shuhguli zake za
kijamii, ikiwemo ujenzi wa Shule, Barabara na huduma za Afya ili
kuhakikisha mambo yanatekelezeka vizuri.

Kaimu mkurugenzi huyo amewaambia wananchi waliokusanyika katika hafla hiyo kwamba, kila mwaka mamlaka imekuwa ikitenga asilimia ya faida inayoipata (bila ya kuitaja) kwa ajili ya kufanya kazi ya kusaidia
miradi mbalimbali ya kijamii, ambayo utolewa ikiwemo elimu, Afya, majanga pamoja na mengineyo, ambayo mamlaka (TPA) inaona yapo ndani ya Sera zake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top