MANCHESTER UNITED YAICHAPA NORWICH CITY 4 - 0. GIGGS KAANZA NA USHINDI MNONO KAMA MENEJA

Timu ya Manchester United imeshinda mchezo wake wa leo dhidi ya Norwich City kwa Ushindi wa Kishindo wa Goli 4 - 0. Ni Wayne Rooney Ndie aliefungua Karamu ya Magoli kwa Kuifungia timu yake bao la Kwanza kwa Mkwaju wa Penati baada ya Walbeck kuchezewa ndivyo sivyo kwenye eneo la hatari na Refa kuamuru ipigwe penati.
Rooney aliweza Kuiandikia Timu hiyo ya Jiji la Manchester Bao la pili pale alipopiga shuti lililomshinda mlinda mlango wa Timu ya Norwich City na Kujaa kimiani na kufanya Matokeo hayo Kuwa 2 - 0 hadi mwisho wa Kipindi cha Kwanza.
Huku Manchester united wakicheza Kandanda Safi leo hii na ikiwa chini ya Kocha wa Muda Ryan Giggs Juan Mata aliyeingia katika Kipindi cha pili alipochukua Nafasi ya Welbeck na Kufunga magoli mawili na kupelekea hadi mwisho wa Mchezo huo matokeo hayo kusomeka 4 - 0.
Ryan Giggs akionesha Uwezo

Vikosi vilikuwa: 
Man Utd: De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia, Carrick, Cleverley (Hernandez 71), Kagawa (Young 65), Rooney, Welbeck (Mata 60).
Subs: Smalling, Lindegaard, Hernandez, Nani, Fletcher.
Goal: Rooney 41pen, 48, Mata 63, 73.

Norwich: Ruddy, Whittaker, Martin, Turner, Olsson, Snodgrass, Howson, Johnson, Redmond (Hooper 69), Fer (Tettey 79), Van Wolfswinkel (Elmander 57).
Subs: Bunn, Gutierrez, Ryan Bennett, Murphy.

Booked: Howson.
Referee: Lee Probert (Wiltshire)

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post