KADINDA ‘AMMISS’ JACK PATRICK

Mwanamitindo maarufu Bongo, Martin Kadinda.

MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda ameonesha hisia zake hadharani baada ya kutupia picha ya rafiki yake kipenzi, modo Jack Patrick mtandaoni na kuonesha kuwa amemkumbuka.
Modo Jack Patrick.
Jack alikamatwa nchini China akidaiwa alikuwa amebeba madawa ya kulevya ambapo kabla hajaondoka, walikuwa wakishirikiana kikazi na mwanamitindo huyo ambaye amemwambia mwandishi wetu kuwa waliishi kama ndugu.
“Jack Patrick alikuwa zaidi ya rafiki, tuliishi vizuri, tumekula good time pamoja na mambo mengine mengi, sitaki kuongelea ishu yake iliyompata lakini kimsingi namkumbuka sana,” alisema Kadinda.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post