Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ na mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ wameingia kwenye bifu zito baada ya kutofautiana katika makubaliano ya kikazi.
Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye mabishano wakati Steve Nyerere alipokuwa akiandaa .
filamu yake mpya iitwayo Get Out ambapo alipaswa kumshirikisha Batuli.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya kuona makubaliano ya kifedha hayazungumziwi.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya kuona makubaliano ya kifedha hayazungumziwi.
“Batuli alipohoji kuhusu malipo, Steve hakuweka wazi ndipo mambo yalipoharibika, kikanuka kisha Batuli akamvaa kwa maneno kiongozi huyo na kudai hana sifa za kuwa kiongozi,” kilisema chanzo chetu.
Ili kujiridhisha na madai hayo, mwanahabari wetu alimwendea hewani Batuli ambapo alipatikana na kukiri kuwa ametofautiana na Steve chanzo kikiwa ni filamu hiyo.
Mwenyekiti wa Bongo Movies, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’.
“Aliponipigia simu nilimwambia sitaweza kwenda kushuti kwa sababu hakuna makubaliano yoyote tuliyofanya ikiwemo gharama, usafiri, mavazi na vinginevyo ndipo akamaindi na kuanza kulaumu na kisha kukata simu,” alisema Batuli.
Ishu haikuishia hapo, taarifa zinadai kuwa baada ya Steve kutofurahishwa na majibu ya Batuli, aliendelea kumtumia meseji za kumlaumu ndipo Batuli alipochachamaa zaidi kwa kujibu mashambulizi.
“Steve anapaswa akasomee utawala na uongozi bora kwani hafai kuwa kiongozi, hana busara, kwa sababu kabla sijagombana naye nilikuwa nikisikia maneno na majungu ila baada ya ugomvi wangu na yeye nimegundua hafai,” alisema Batuli na kuongeza:
“Ananiambia mimi ni msanii mchanga ilihali mimi kwenye kiwanda nipo kwa miaka kumi na nne na mwaka 2,000 wakati naanza yeye alikuwa anachekesha watu ili apate kula kwanza nimemdharau kwa sababu amekuwa akinichonganisha na wasanii wa Bongo Movie eti mimi nimewaambia wanajiuza.”
Baada ya Batuli kufunguka, gazeti hili lilimgeukia Steve Nyerere na kumsomea madai hayo ambapo alifunguka:
“Sipendwi na watu na sijui nini tatizo, nikiwa kama dairekta nina uwezo wa kumchagua huyu nifanye naye kazi na huyu kumuacha, yule (Batuli) kama analeta chuki basi zitakuja hivyo basi ni nyingi tu,’’ alisema Nyerere na kuongeza:
“Kwa heshima niliyoitengeneza kwa miaka 32 alafu nije nigombane na mwanamke, kwanza nagombana naye nini? Nashukuru nimepata ushauri, naendelea na kazi ya kutetea maslahi ya Bongo Muvi kama ni filamu mimi nilishachezesha msanii mwengine.”
>>GPL
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.