Unknown Unknown Author
Title: BODA BODA WAPEWA MAFUNZO NA KUPIMA AFYA MKOANI LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa chama cha Madereva Bodaboda Mahumbika akipokea Cheti cha Kufuzu Mafunzo ya udereva kutoka kwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi ...

VYETI BODA BODAMwenyekiti wa chama cha Madereva Bodaboda Mahumbika akipokea Cheti cha Kufuzu Mafunzo ya udereva kutoka kwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Ndg Renatha Mzinga.VYETI BODA BODA.6Meneja wa CHF Mkoa wa Lindi Ndg Fortunata Kullaya akitoa somo kwa kwa madereva bodaboda waliofuzu mafunzo ya udereva kijiji cha mahumbikaVYETI BODA BODA.7Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Ndg: Abdulaziz akipima afya wakati wa hafla ya utoaji vyeti wa madereva bodaboda kijiji cha mahumbika

ABDULAZIZ -Lindi
Mfuko wa Afya Ya Jamii (CHF)Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa
wa Lindi wamewezesha kupimwa kwa Afya za Madereva Boda boda wa kata ya Kiwalala wilayani Lindi baada ya kufuzu mafunzo ya Udereva
yaliyotolewa chini ya Mpango shirikishi wa Polisi Jamii Mkoani Humo.

Akiongea na madereva Boda boda mara baada ya kuwatunuku vyeti vya
kufuzu mafunzo hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna
Msaidizi, Renatha Mzinga ametoa wito kwa wahitimu hao kujali afya zao
kila wakati ambapo aliwahimiza kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii ili
kupunguza gharama za Tiba kwa Mwaka.

Aidha Kamanda Mzinga aliwataka kutii Sheria za Usalama barabarani na
kuacha kuendeshwa na Abiria anaemchukua Kwa Usalama wa maisha yaoVYETI BODA BODA.5
“Najua sasa ni madereva makini baada ya kupewa mafunzo haya na leo kuwakabidhi vyeti vyenu ninahakika sasa Utoendeshwa na abiria wako fuata sheria kila wakati na ujenge Tabia ya Ya Urafiki na Askari tofauti na ilivyo kwa madereva wengi kuogopa askari kwa kuwa wanavunja sheria kwa makusudi" alimalizia Kamanda Mzinga.

Awali Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Lindi, Fortunata Kullaya alieleza kuwa kupitia Mpango wa CHF tayari ofisi yake imeanza Utaratibu wa kuyafikia makundi mbalimbali katika Programu ya Kata kwa kata ambapo utoa vipimo Bure kupitia madaktari Bingwa wanaoongozana naoVYETI BODA BODA.3“Mfuko wa CHF sasa ndio mkombozi wenu ndugu zangu kwa kuwa unajiunga kwa pesa ndogo na unatibiwa kwa watu 6 (kaya) kwa Mwaka tumieni fursa hii muhimu na kama ulivyoona leo tumeamua kuja kuwapima Bure ili nanyi mjue afya zenu na hii itasaidia kupata Tele kwa tele katika zahanati zenu toka serikali kuu"Alisema KullayaVYETI BODA BODA.2Jumla ya waendesha Bodaboda 29 waliohitimu mafunzo ya kuendesha
bodaboda walikabidhiwa Vyeti na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi na
baadae kupata Fursa ya kupimwa magonjwa mbalimbali na kupata Ushauri wa Afya chini ya Mpango wa Kuhamasisha Jamii Kujiunga Na CHF pamoja na Tiba Kwa Kadi Mkoani Lindi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top