Zoezi la kuwatafuta watu waliokuwa hawajaonekana kutokana na ajali ya boti ya kilimanjaro II imeendelea tena leo kwa kuzishirikisha boti mbili za wananchi moja ya kikosi cha KMKM, Polisi na Tagi ya bandari.
Hadi saa saba mchana hakuna mwili wowote uliokuwa umepatikana kwa mujibu wa mkurugenzi wa mamlaka ya usafiri baharini Abdi Omar Maalim.
Amesema boti ya tagi na polisi zimetafuta zaidi katika bahari kuu na zimerejea bila mafanikio licha ya kukuta baadhi ya mizigo tu ikielea huku boti nyengine ndogo ndogo zikiendelea na utafutaji.
Amesema kuwa kuna tetesi baadhi ya abiria waliomo katika menifesto za waliosafiri hawakupanda boti hiyo wakati ikiondoka mkoani habari ambazo amesema wanazifuatilia ili kujua ukweli wake ila amesema zipo familia zilizofika hapo na kutoa taarifa ya kutokuwaona ndugu zao wasiopungua wananae.
Kuhusiana na usafiri wa bahari uliozuiliwa kwa siku ya jana kutokana na kuwa na hali mbaya ya hewa leo hii zimeruhusiwa kuendelea na safari zao kama kawaida baada ya kuwasiliana na mamlaka ya hali ya hewa na kupata taarifa ya usalama kwa siku ya leo.
Miili ya watu watano imeopolewa wakiwa wamefariki katika ajali ya boti hiyo iliyopata misukosuko kutokana na dharuba na mawimbi makali wakati ikitokea kisiwani Pemba kuelekea Malindi kisiwani Unguja mapema jana asubuhi
VIA STARTV HABARI
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.