MAUAJI YA WALINZI WAWILI KITUO CHA MAFUTA CHA KOBIL– MINGOYO,LINDI

DSCF4679Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Mnazi mmoja wakishuhudia mauaji yaliyo tokea kituoni hapo usiku wa kuamkia leo.DSCF4691Maafisa Polisi wakifanya uchunguzi katika kituo hicho kilichotokea Mauaji ya Walinzi wa Kituo Hicho Cha Mafuta cha KOBIL Mnazi mmoja-Lindi
NA. Abdulaziz,Lindi
Walinzi wawili Ambao walikuwa walinzi wa Kituo cha Mafuta cha Kobil kilichopo Mnazi mmoja Kata ya Mingoyo Manispaa ya Lindi wameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi ambapo walifanikiwa kuvunja kituo hicho lakini walishindwa kupata fedha baada ya kushindwa kuvunja/kubeba(self)huku wakiitelekeza kichakani bunduki aina ya Short Gun ya walinzi hao.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni mfululuzo wa mauaji ya walinzi wa vituo vya mafuta yaliyotokea siku za hivi karibuni, Tukio limetokea Usiku wa kuamkia leo na kubainika asubuhi baada ya Meneja wa kituo hicho ,Bw Saidi Ally Rashid kukuta walinzi hao wakiwa wamelala wakivuja damu
Walinzi hao waliopigwa na kufariki papo hapo walifahamika kwa jina la Selemani Mohamed Mchawi na Mohamed Twalib wote wakiwa ni wakazi wa Mingoyo
Akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika eneo la tukio, Meneja wa Kituo hicho cha Mafuta cha Kobil, Saidi Ally Rashid Alibainisha kuwa majira ya saa 12 Asubuhi alifika hapo kituoni kama ilivyo kawaida huwakuta walinzi na kumkabidhi kituo
DSCF4699Waandishi yaani leo nimeona ajabu nafika simuoni hata mlinzi mmoja nikiangalia mlango wa Shell uko wazi kioo kimevunjwa…Nilipozunguka zaidi nilikuta walinzi wakiwa wamelala wakivuja damu na Kwa Ishara nilibaini wamekufa..Nilishtuka sana na nilikimbilia kituo cha Polisi kwa taarifa zaidi ya nilichoona asubuhi hii’ Alimalizia Saidi
Naye Ndugu wa mmoja wa Marehemu ambae pia ni Diwani wa Kata ya Mingoyo lilipotokea tukio hilo, Jamaldin Mandowa kwa Upande wake licha kupokea kwa masikitiko kutokea kwa Tukio hilo alitoa wito kwa Wanajamii kuwa makini na Wageni wanaofika katika maeneo yao ikiwemo Nyumba za kulala wageni pamoja na kwenye Ma bar kufuatia kuongezeka kwa Wageni wengi kutokana na Fursa zilizopo Mkoa wa Lindi na Mtwara
Kufuatia tukio hilo lililosababisha mauaji hayo Wezi hao walifanikiwa kuvunja kituo hicho lakini walishindwa kupata fedha kufuatia Uimara wa kitunza fedha katika kituo hicho sambamba na Tukio hilo hivi karibuni walinzi watatu wa vituo vya mafuta vya Mtama, Nanganga na Newala waliuliwa na kufanikiwa kuiba fedha walizozikuta.





Previous Post Next Post