JE ULIMISS SIRI YA MTUNGI SEHEMU YA TATU? IANGALIE HAPA (with English Subtitles)

Stephen, mdogo wake Duma amekuwa mtoro shuleni. Duma analifahamu hili kwa mara ya kwanza pale Mwalimu Mkuu anapompa sharti la mwisho la ama Stephen ajirekebishe au afukuzwe shule. Duma analazimika kujifaragua ili kumsaidia mdogo wake.
Biashara ya Cheche haina maslahi kama ambavyo ingetakiwa iwe na Mwanaidi, anapata wasiwasi kwa jinsi mkwewe anavyompuuza Cheusi.
Wakati huo huo, pale Nusura anapogongwa na bajaji nje ya karakana ya Kizito, ajali hii inaibua mfululizo wa matukio ya kushangaza. Mzee Kizito anamuita mjomba wake Mawazo aje kusawazisha mambo!

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post