AJALI KAZINI? AU UZEMBE KAZINI?

379340_10151436822449339_1478613055_nFundi wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Iringa, Selemani Mbuma akiwa amenaswa na umeme baada ya wenzake kuwasha umeme kimakosa wakati akiendelea na matengenezo katika eneo la Mlandege mkoani humo.

Matatizo haya hujitokeza mara kwa mara Je swali la kujiuliza huwa hawawasiliani pindi wanapotaka kurudisha umeme huo? au hakuna fundi in charge ambaye ndio kiongozi wa msafara wa ufundi ambaye ndie atakaye husika na miongozo yote ya kuhakikisha kuwa hakuna mtu anaye endelea na matengenezo ndio umeme uwashwe? jibu naweza jipa mwenyewe kuwa lazima awepo ila ni Ufanyaji kazi wa mazoea na kuwaamini sana hawa wanaoitwa saidia kuwapa majukumu yaliyokuwa makubwa kuliko uwezo wao na ndio makosa kama haya yanatokea, maisha ya mtu yanapotea kwa uzembe wa kizembe kama huu.

Picha na Geofrey Nyang’oro

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post