Unknown Unknown Author
Title: KARIAKOO FC WAICHAPA GENERATION YA NACHINGWEA 1 - 0
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha Kariakoo Fc kilichocheza na kuishinda Generation Fc ya Nachingwea. Timu ya Kariakoo Fc leo imeshuka dimbani kumenyana na Ti...
DSC04796Kikosi cha Kariakoo Fc kilichocheza na kuishinda Generation Fc ya Nachingwea.
Timu ya Kariakoo Fc leo imeshuka dimbani kumenyana na Timu ya Generation Fc ya Wilayani Nachingwea katika kutafuta bingwa wa kucheza ligi daraja la kwanza.
Mechi hiyo iliyoshuhudiwa na washabiki lukuki wa mji wa lindi ilikuwa inafikiriwa kuwa ya mvuto zaidi kwani timu hizi ni timu ambazo zimefuzu kutoka katika mizunguko iliyopita hivyo wate ni mabingwa hivyo ilitegemewa kuonekana soka safi lililolakiufundi zaidi, lakini hali haikuwa hivyo kwani Timu ya Generation walijikuta wakicheza soka la mabavu kwani walicheza rafu nyingi sana na refa aliwajenga kwa kutowapatia kadi yeyote ya Manjano katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
DSC04794Salum Abdillah aliiwezesha timu yake ya Kariakoo kuongoza baada ya kupata pasi nzuri ambayo aliitanguliza kwa mbele na kumchungulia kipa wa Generation amekaaje na kuachia shuti ambalo lilimpita Golikipa huyo mikononi mithili ya mshale. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Kariakoo walikuwa Mbele kwa goli hilo moja na wakiwa wamepoteza nafasi kadhaa za wazi za kufunga.
Kipindi cha pili kilianza kwa kufanya mabadiliko mbalimbali lakini mabadiliko hayo yalikuwa faida kwa Generation kwani walionesha uhai kwa kuweza kufika langoni mwa Kariakoo lakini beki ziliweza kuwathibiti na kushindwa kufurukuta.
Generation walianza kucheza rafu za wazi ambazo zilishindwa kuvumilika na mwamuzi kumtoa kwa kadi nyekundu captain wa timu hiyo. pia waliendelea na mchezo huo mbaya lakini bado refa hakuweza kuwaadhibu kwa mara nyingine hiyo ilitokana na kuzongwa na wachezaji hao pale aliipokuwa anataka kutoa maamuzi yake. hadi mwisho wa mchezo Matokeo yalibaki kuwa Kariakoo 1 – 0 Generation.

About Author

Advertisement

 
Top