Tabora. Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, imekamilisha usikilizaji wa awali wa pingamizi zilizowasilishwa katika shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Kigoma Kusini, yaliyowasilishwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, David Kafulila.
Jaji wa Mahakama hiyo, Sam Rumanyika akiahirisha shauri hilo juzi, aliwaambia mawakili wa pande zote kuwa kufuatia kumalizika kwa mapingamizi kinachofuata ni kupeleka jalada hilo kwa Jaji Kiongozi, ili aweze kupanga jaji wa kusikiliza shauri mama.
Akizungumza nje ya mahakama, wakili wa Kafulila, Daniel Lumenyela alisema hatua iliyofikiwa ni nzuri kwa upande wao, na anaamini jaji yoyote atakayepangiwa kusikiliza shauri hilo atatenda haki na kumpa ushindi mteja wake aliodai kuupata katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Alisema wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo wamemtaka msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo atoe matokeo sahihi, alete nakala halisi za vituo vyote 382, aje na nakala halisi ya fomu namba 21b na nakala ya matokeo ya majumuisho ya vituo vyote.