Unknown Unknown Author
Title: HALI MBAYA YA KIAFYA YAMFANYA KOCHA HARRY REDKNAPP KUACHAKUIFUNDISHAI QPR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Harry Redknapp ameachia ngazi Queens Park Rangers kufuatia maumivu ya magoti lakini ameweka wazi kuwa bado huo hautakuwa mwisho wak...
Harry Redknapp
Harry Redknapp ameachia ngazi Queens Park Rangers kufuatia maumivu ya magoti lakini ameweka wazi kuwa bado huo hautakuwa mwisho wake wa kufundisha soka.
Redknapp, 67, amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuambiwa kuwa atahitajika kufanyiwa upasuaji wa magoti yake yote mawili. Hawezi kutembea hata hatua 100, akakiri kuwa kwa sasa yeye si mtu sahihi wa kuiongoza QPR katika vita vya kushuka daraja. Akampigia mmiliki wa timu saa 11.30 alfajiri na kumjulisha habari hizo.
Kocha huyo mkongwe anasema: “Sikupata usingizi usiku mzima, nawaza kuhusu hilo. Siwezi kutembea, nimekuwa kwenye maumivu muda wote. Nimejitahidi sana lakini inafika hatua nakuwa siwezi kufanya kazi yangu.
“Siwezi kwenda uwanjani, hata kama gari litaniingiza mpaka ndani lakini bado nitapaswa kutembea kidogo.
“Nilikwenda uwanjani kumtazama mjukuu wangu akicheza soka wikiendi iliyopita lakini baada ya dakika tano tu nililazimika kurudi kwenye gari. Sikuweza hata kusimama. Ni maisha gani haya kama huwezi hata kutazama watoto wakicheza? Nikafikiria usiku kucha, baadae nikaamua kumipigia Tony Fernandes.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top