Unknown Unknown Author
Title: RAIS ZUMA AAPISHWA KWA MUHULA WA PILI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameapishwa kwa muhula wa pili wa uongozi. Maelfu ya wafuasi, wakipepea bendera za taifa, walishangili...
Rais Jacob Zuma akiapishwa

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameapishwa kwa muhula wa pili wa uongozi.
Maelfu ya wafuasi, wakipepea bendera za taifa, walishangilia ndege za jeshi za Afrika Kusini zilipopita juu ya uwanja wa sherehe.

Rais Jakaya Kikwete

Viongozi wa nchi 20 walikuwako katika sherehe hiyo pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.

Katika hotuba yake ya kutawazwa Rais Zuma aliahidi kuwa serikali yake itakuza uchumi na nafasi za ajira. Chama chake cha ANC kilishinda uchaguzi awali mwezi huu ambapo kilipata kura zaidi ya asili-mia-60.
Hii ni mara ya tano kwa chama cha ANC kushinda katika uchaguzi na kimeongoza nchi tangu utawala wa ubaguzi wa rangi kumalizika.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top