Unknown Unknown Author
Title: CECAFA NILE BASIN: MBEYA CITY YAANZA VYEMA YAICHAPA ACADEMIA TCHITE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
RIPOTI toka huko Khartoum, Sudan zimesema Wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye Michuano ya CECAFA NILE BASIN, Mbeya City, Leo hii wameanza ...
Mbeya City
RIPOTI toka huko Khartoum, Sudan zimesema Wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye Michuano ya CECAFA NILE BASIN, Mbeya City, Leo hii wameanza vyema Mashindano hayo kwa kuichapa Academie Tchite ya Burundi Bao 3-2 kwenye Mechi ya KUNDI B.

Kwenye Mechi hii, Bao za Mbeya City zilifungwa na Paul Nonga, Mwegane Yeya na Themi Felix.

Hapo Jana, Timu ya Zanzibar, Polisi, ilichapwa Bao 3-0 na Wenyeji Al-Merreikh ya Sudan.

Kufuatia kujitoa kwa Timu 5 katika Dakika za mwisho, CECAFA iliamua kubadilisha Makundi na Ratiba ya Mashindano haya.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa CECAFA, Rogers Mulindwa, Timu zilizojitoa ni pamoja na Wageni Waalikwa maalum, Klabu za Egypt Al Masry na Arab Contractors.
Nyingine ni Elman ya Somalia na Klabu ya Sudan, Hey Al Arab.

RATIBA/MATOKEO

Ijumaa Mei 23


Victoria University (Uganda) 1 - 0 Malakia (South Sudan)

Al-Merreikh [Sudan] 3 - 0 Police [Zanzibar]

Al-Shandy [Sudan] 2 - 1 Dkhill [Djibouti]

Jumamosi Mei 24

Mbeya City [Tanzania] 3 - Academie Tchite [Burundi] 2

AFC Leopards [Kenya] v Etincelles [Rwanda]

Hali hiyo imefanya Timu kubakia 11 na Makundi kuwekwa kuwa Matatu.

KUNDI A

-Polisi [Zanzibar]
-Victoria University Uganda]
-Malakia [South Sudan]
-Al Merreikh [Sdan]

KUNDI B

-Mbeya City [Tanzania Bara]
-AFC Leopards [Kenya]
-Academie Tchite [Burundi]
-Enticelles [Rwanda]

KUNDI C

-Defence [Ethiopia]
-Dkhill FC [Djibouti]
-Al Shandy [Sudan]
>>Soka In Bongo

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top