Unknown Unknown Author
Title: BANDA AAGIZA KUSITISHA ZOEZI LA KUHESABIWA KURA NA UCHAGUZI URUDIWE-MALAWI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais Joyce Banda wa Malawi ameamuru kusitishwa mara moja kwa shughuli ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ...
Joyce Banda
Rais Joyce Banda wa Malawi ameamuru kusitishwa mara moja kwa shughuli ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ulifanyika jumanne iliyopita.

Akizungumza Ikulu mjini Lilongwe mapema leo hii ameiamuru Tume ya uchanguzi MEC kusitisha shughuli hiyo na kutangaza kuwa uchaguzi urudiwe ndani ya siku 90 kutoka leo na kwamba yeye hatogombea tena urais wa nchi hiyo.

Wagombea kiti cha Urais Malawi
Baadhi ya viongozi wanaowania urais nchini Malawi

Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amearifu kutoka mjini Lilongwe kuwa Dr Banda amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na kile alichokiita kuvurugwa kwa mtiririko mzima wa shughuli za upigaji kura, kuhesabu na hata namna ya kusimamia utoaji wa matokeo yake.

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Malawi Jaji Mackson Mbendera amesema kuwa anawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kuangalia uwezekano wa amri hiyo ya Rais kutekelezwa na kama haijavunja sheria ya nchi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top