Unknown Unknown Author
Title: WAZIRI MKUU ATOA AGIZO HILI KWA TAASISI ZA UMMA, AGIZO KUTEKELEZWA NDANI YA MIEZI MINNE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua mtandao wa 4G LTE wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kwenye viwanja vya...
4G LTE
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua mtandao wa 4G LTE wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017.
4G LTE
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Spika wa Bunge Job Ndugai (wapili kushoto) na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Mtandao wa 4G LTE wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Zhang Yongquan na kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka taasisi mbalimbali za umma zinazodaiwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ziwe zimelipa madeni yao ifikapo Juni 30, mwaka huu.

TTCL inazidai taasisi mbalimbali za umma jumla ya sh. bilioni 11.5 ikiwa ni gharama ya huduma walizozitoa kwa taasisi hizo, hivyo kukwamisha utendaji wa kampuni hiyo.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, 10 Februari, 2017) wakati akizindua huduma za simu ya mkononi kwa teknolojia ya 4G LTE ya TTCL mjini Dodoma.

Pia amemtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akutane na wadaiwa sugu wote wathibitishe madeni husika na kisha wapange namna ya kulipa.
“Nijuavyo, kila Wizara inatenga bajeti kwa ajili ya ankara za simu, sasa haya malimbikizo yanatoka wapi?. Ni lazima wadaiwa wote walipe madeni yao mara moja,” ameagiza.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa “unapokuwa na deni lazima ulipe. Mheshimiwa Waziri simamia hili, na unipe taarifa ya utekelezaji kabla ya Mkutano ujao wa Bunge la Bajeti,”.

Pia Waziri Mkuu alitoa rai kwa Menejimenti na watumishi wa TTCL kwa kuwataka watambue dhamana waliyopewa na waitendee haki kwa kufanya kazi kwa bidii na weledi.

“Fanyeni kazi kwa bidii, weledi, uzalendo, maarifa na ubunifu wa hali ya juu. Imarisheni Idara ya Masoko, hamasisheni ubunifu kwenye Kampuni na wapeni nafasi vijana wenye uwezo,”
.

“Kama hiki ni kizazi cha T, wacha kizazi hicho kiongoze mapinduzi ya T, muhimu uzalendo, uwezo, dhamira na ubunifu vizingatiwe katika kutoa nafasi hizo,”. amesisitiza.

Pia amewataka viongozi wa TTCL wapitie upya muundo wake na wajiridhishe kama unaendana na ushindani wa kibiashara na dhamira ya Serikali ya kupunguza gharama zisizo za lazima.

Akizungumzia suala la idadi ya watumishi wa Kampuni, Waziri Mkuu ameshauri wajifanyie tathmini wenyewe kujua mahitaji halisi ya watumishi na kufanya maamuzi kwa kuzingatia sheria za nchi.
“Serikali inatarajia TTCL ijiendeshe kwa faida na sio kuja kuiomba Serikali ruzuku, hivyo hamna budi kupunguza gharama za uendeshaji wa kampuni kwa kadiri inavyowezekana,” amesema.

Awali, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba alisema miongoni mwa changamoto zinazokabili kampuni hiyo ni pamoja na mtaji mdogo.

Pia aliiomba Serikali iwasaidie ili waweze kulipwa madeni yao wanayozidai taasisi mbalimbali za umma kutokana na huduma walizozitoa kwa taasisi hizo.

Hata hivyo Bw. Kindamba ameahidi kwamba watafanya kazi kwa biidi ili kuhakikisha TTCL inaongoza kwa kutoa huduma bora za mawasiliano nchini.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top