Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA WILAYA YA KILWA APIGA MARUFUKU UINGIZAJI WA MIFUGO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow. Kilwa KATIKA kukabiliana na migogoro baina ya wafugaji na wakulima. Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Christopher Ngub...
Na. Ahmad Mmow. Kilwa
KATIKA kukabiliana na migogoro baina ya wafugaji na wakulima. Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Christopher Ngubiagai amepiga marufuku uingizaji wa mifugo wilayani humo hadi ufanyike uhakiki wa mifugo iliyopo wilayani humo.
mifugo
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngea, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kijiji hicho. Mkuu huyo wa wilaya alisema uamuzi huo unatokana na hali iliyoanza kujitokeza wilayani humo baina ya wakulima na wafugaji. Kutokana na idadi kubwa ya mifugo kuwepo katika maeneo ambayo sio miongoni mwa yanayositahili kufugia.

Ngubiagai alisema kutokana na wingi wa mifugo iliyopo katika maeneo yasioruhusiwa na kutokuwa na uhakika wa idadi ya mifugo iliyopo kumeanza kuzuka migogoro ambayo isipodhibitiwa inaweza kusababisha uvunjifu wa amani wilayani humo.
"Ni bora wilaya ya Kilwa ikasitisha kwa muda uingizaji wa mifugo kwamakundi ili kutoa mwanya wa kushugulikia na kutatua matatizo yaliyosababishwa nakuwa na mifugo katika maeneo ambayo hayakuruhusiwa na halmashauri ya wilaya yapokee mifugo," alisema Ngubiagai.

Mkuu huyo wa wilaya ya Kilwa alisema uamuzi huo unatokana na mapendekezo ya kamati iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi ambayo pamoja na mambo mengine ilichunguza chanzo na sababu za migogoro ya wakulima na wafugaji iliyoanza kujitokeza wilayani humo. 

Alisema kwa kuwa kamati hiyo ilibaini upungufu katika mipango ya matumizi bora ya ardhi ambao umechangia kuwepo migogoro, ni vema halmashauri ya wilaya hiyo kupewa muda wa kufanya rejea ya mipango hiyo haraka badala kuendelea kupokea mifugo bila kuwa na mipango madhubuti.

Pamoja na katazo hilo, mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kilwa alitaja baadhi ya mikakati na hatua zinazopaswa kuchukuliwa kabla ya kuruhusu mifugo kuendelea kuingizwa.

Miongoni mwa mwa hatua na mikakati hiyo ni kuimarishwa kwa udhibiti wa uingizaji wa mifugo. Ikiwa ni pamoja na kufanya rejea ya sheria kuu na kutunga sheria ya halmashauri ili kudhibiti misafara ya mifugo baina ya vijiji vilivyopo katika wilaya hiyo, kuimarishwa utunzaji takwimu za mifugo inayoingia na kutoka wilayani humo kwa kutumia mfumo wa kiilektrotoniki na kubaini njia zisizo rasimi zinazotumika kuingiza na kupitisha mifugo katika wilaya hiyo ili zidhibitiwe haraka.

Aidha aliwataka wakulima wanaoishi katika maeneo yaliyotengwa kwaajili ya ufugaji na wafugaji wa naoishi katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo waondoke kutoka katika maeneo hayo. Huku akihaidi kuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi na watendaji watakaobainika walipindisha taratibu na sheria na kusababisha mifugo kuingizwa na kupelekwa katika maeneo yasioruhusiwa.
"Migogoro inachangia kukwamisha shuguliza za maendeleo kufanyika, haiwezekani sheria zipo wazi lakini mifugo iwe inazagaa, baadhi ya watendaji na viongozi wanashiriki na kuchangia hali hii, tutashugulika nao," alisisitiza Ngubiagai.

Awali baadhi ya wananchi walimueleza mkuu huyo wa wilaya kwamba ingawa sio kijiji hicho sio miongoni mwa vijji vilivyokubali kupokea mifugo, hata hivyo kinamifugo ambayo haileweki iliingia kwa idhini ya nani. Miongoni mwa waliozungumza ni Ali Kinunga. Ambae alisema hali katika kijiji hicho na kata mzima ya Mitole ni mbaya. 

Akitahadharisha kwamba serikali isipochukua hatua za haraka za kuwaondoa wafugaji kunaweza kutokea uvunjifu wa amani.
"Hifadhi za misitu zinaharibiwa, vyanzo vya maji ikiwamo bwawa la Maliwe lipo hatarini kukauka. Mazao mashambani yanaliwa tunapambana na wanyama waharibifu na mifugo," alisema Kinunga.

Nae Mariamu Ahmad, alisema kijijiji hicho kinaweza kukumbwa na njaa iwapo serikali haitachukua hatua za haraka za kuondoa mifugo hiyo.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top